![]() |
| Askofu Zachary Kakobe |
Nyakati tulizonazo leo,zinzitwa NYAKATI ZA HATARI..Biblia inasema kwamba siku hizi za mwisho,wengine watajitenga na imani,wakisikiliza ROHO ZIDANGANYAZO na MAFUNDISHO YA MASHETANI (2TIMOTHEO 3:1,1TIMOTHEO 4:1).
Roho zidanganyazo zitafanya kila namna,kutudanganya,ili kile cha Mungu tukiite cha shetani,na kile kilicho cha shetani,tukiite cha Mungu.Leo,tunazungukwa na watu wanaosema,jihadhari usiende kule.
Ingawa kuna miujiza mingi huko,miujiza hiyo,inatokana na ROHO CHAFU au MASHETANI.Mtu yule,anatoa pepo kwa kutumia DAWA au HIRIZI.Kutokana na mambo yake ya ushirikina,mtu akienda kumsikiliza mara moja tu,yeye naye ananyweshwa roho chafu na kudanganyika.
Maneno haya,yanaweza yakawa ya kweli au yasiwe ya ukweli.Pasipokuwa na mafundisho,hatuwezi kupambanua kilicho cha Mungu na kilicho cha Shetani.Pasipo kutopambanua,tunaweza tukamwita mtu wa Mungu kuwa ni PEPO na kwamba anatoa pepo kwa BEELZEBULI,mkuu wa pepo,kwasababu tu HAFUATANI NASI (YOHANA 8:48-49; MATHAYO 12:22-24;LUKA 9:49-50).
Mambo haya,hayapaswi kuwa hivi.Kwa sababu hii basi ni makusudi ya Mungu ujifunze somo hili.Tunaligawa somo hili katika vipengele vitatu;-
Roho zidanganyazo zitafanya kila namna,kutudanganya,ili kile cha Mungu tukiite cha shetani,na kile kilicho cha shetani,tukiite cha Mungu.Leo,tunazungukwa na watu wanaosema,jihadhari usiende kule.
Ingawa kuna miujiza mingi huko,miujiza hiyo,inatokana na ROHO CHAFU au MASHETANI.Mtu yule,anatoa pepo kwa kutumia DAWA au HIRIZI.Kutokana na mambo yake ya ushirikina,mtu akienda kumsikiliza mara moja tu,yeye naye ananyweshwa roho chafu na kudanganyika.
Maneno haya,yanaweza yakawa ya kweli au yasiwe ya ukweli.Pasipokuwa na mafundisho,hatuwezi kupambanua kilicho cha Mungu na kilicho cha Shetani.Pasipo kutopambanua,tunaweza tukamwita mtu wa Mungu kuwa ni PEPO na kwamba anatoa pepo kwa BEELZEBULI,mkuu wa pepo,kwasababu tu HAFUATANI NASI (YOHANA 8:48-49; MATHAYO 12:22-24;LUKA 9:49-50).
Mambo haya,hayapaswi kuwa hivi.Kwa sababu hii basi ni makusudi ya Mungu ujifunze somo hili.Tunaligawa somo hili katika vipengele vitatu;-
- UWEZEKANO WA SHETANI KUFANYA MIUJIZA.
- JINSI YA KUIFAHAMU MIUJIZA YA MUNGU.
- HUKUMU YA WATUMISHI WA SHETANI
1.UWEZEKANO WA SHETANI KUFANYA MIUJIZA.
Shetani, ana uwezo wa kufanya ishara na miujiza kadhaa,kwa kipimo kidogo
cha uwezo ulio na mpaka.Roho chafu,roho za mashetani,zina uwezo wa
kufanya ishara (UFUNUO 16:13-14).Wakati wa dhiki kubwa,roho za mashetani,zitafanya ishara kubwa,hata kufanya moto kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu (UFUNUO 13:11-13).Wakati wa wana wa Israeli, walipokuwa hawajatoka Misri,waganga na wachawi wa Farao,walifanya miujiza kwa uwezo wa Shetani:-
(a). Wachawi hao,walipozibwaga fimbo zao chini,ziligeuka kuwa
nyoka kwa mfano wa muujiza alioufanya Mungu kwa kuwatumia Musa na
Haruni (KUTOKA 7:8-12).
(b) Wachawi hawa,walifanya muujiza wa kubadili maji kuwa damu,kwa mfano wa muujiza alioufanya Mungu kwa kuwatumia Musa na Haruni (KUTOKA 7:19-22)
Hata hivyo,pamoja na wachawi na waganga hawa kufanya miujiza
hii,walikuwa na mpaka katika uwezo wao.Wachawi hawa,walishindwa kufanya
mavumbi ya nchi kuwa chawa kwa mfano wa Musa na Haruni,na vulevile
walishindwa kuzuia majipu yaliyosababishwa na muujiza wa Mungu kupitia
kwa Musa,kuwapata na wao pia.Wakakiri kwamba uwezo wa Mungu uko juu mno
kuliko uwezo wao (KUTOKA 8:16-19;9:8-11).Shetani hana uwezo
wote,hawezi kutenda mambo yote.Mungu wetu ana uwezo mkuu mno.Fimbo ya
Haruni,ilizimeza fimbo za wachawi,kudhihirisha uwezo wa Mungu ulivyo
mkubwa mno kuliko majeshi yote ya Shetani(KUTOKA 7:11-12).Ni muhimu kufahamu kwamba miujiza ya Shetani,inalengo laKUWAPOTEZA,kama yamkini hata walio wateule.Ni nguvu ya upotevu,ya kuwafanya wale wote wasioipenda kweli ya Neno la Mungu KUPOTEA (MATHAYO 24:24;2WATHESALONIKE 2:7-12).Ili
basi tusipotezwe na roho hizi za mashetani,ni muhimu kuifahamu
Kweli,ili tuweze kupambanua miujiza ya mashetani na miujiza ya
Mungu.Hili sasa linatuleta katika kipengele cha pili cha somo letu.
2. . JINSI YA KUIFAHAMU MIUJIZA YA MUNGU.
Ili kuifahamu na kuipambanua miujiza ya mashetani.itakuwa vema kujifunza
alama zitakazotuwezesha kuifahamu miujiza ya Mungu.Tukiweza kufahamu
namna ya kupambanua miujiza ya Mungu,itakuwa ni rahisi kufahamu kinyume
chake,na kuifahamu miujiza ya mashetani.ZIKO ALAMA KUMI (10) za
kutuwezesha kuifahamu miujiza ya Mungu.Alama zote hizi,lazima zionekane
katika huduma yoyote inayotumiwa na Mungu kufanya miujiza.Tukiziona
alama zote hizi kumi katika huduma yoyote ya miujiza,tujue huduma hiyo
niya Mungu,na hatupaswi kusema mtu huyo wa Mungu anatumia roho chafu au
anatoa pepo kwa Beelzebuli,mkuu wa pepo.Alama hizi kumi ni hizi
zifuatazo:-
1. .Mtu anayetumiwa kufanya miujiza ya Mungu, lazima mwenyewe awe
ameamini na kuokolewa; akikiri mwenyewe wokovu ulio katika Kristo Yesu,
na kuushuhudia ishara au miujiza ya Mungu, hufuatana nao WAAMINIO tu, au waliookolewa (MARKO 16:17).Mtu
yeyote ambaye hajaokoka, hawezi kufanya miujiza inayotokana na
Mungu.Miujiza anayoifanya mtu yeyote ambaye hajaokoka, ni miujiza ya
shetani.
2. .Huma yoyote ya miujiza ya Mungu, lazima iambatane na
Biblia au Neno la Mungu, kwa kuwa Neno la Mungu ndiyo dawa ya ugonjwa
na tena ndilo linalofanya miujiza(ZABURI 107:20; MITHALI 4:20-22; YOHANA 6:63).
Mtu anayetumiwa kufanya miujiza ya Mungu, ataiamini Biblia na kuifanya
kuwa msingi wa utendaji wake wote. Huduma yoyote ya miujiza
isiyoambatana Biblia, inatokana na Shetani.
3. Huduma yoyote ya miujiza inayotokana na Mungu, LAZIMA iambatane na KUHUBIRI NA KUFUNDISHA Neno
la Mungu. Mtu yeyote anayedai kwamba yeye hakupewa kuhubiri Neno, ila
amepewa karama ya kutenda miujiza tu, huyo anatumiwa na Shetani (LUKA 4:18; 5:17; 9; 8:1-2; MATHAYO 10:7-8). Huduma
yoyote ya miujiza ya Mungu, lazima iambatane kuhubiri kwamba watu
watubu dhambi zao na kuziacha, na kuokolewa. Kinyume cha hapo, ni huduma
ya Shetani (MARKO 4:6;12-13).
4. Miujiza yoyote ya Mungu, LAZIMA ifanyike kwa jina la YESU (LUKA 10:17; MATENDO 4:30; MARKO 16:17; MATENDO 3:6; 4:10; 3;13, 16, 16:18).
5. Miujiza yoyote ya Mungu, hutumika kuwaleta watu kwa Bwana Yesu
na kuwafanya wawe wanafunzi wa Yesu, na kuwafundisha kudumu katika
kanisa linalohubiri wokovu (MATENDO 5:12, 14; 2:41-43; 6:7-8; 8:5-8, 12). Miujiza isiyo na lengo hili ni miujiza ya Shetani.
6.
Mtu yeyote anayetumiwa kufanya miujiza ya Mungu, lazima afanye huduma
yake kwa kushirikiana na makanisa yanayohubiri wokovu, ili apate kutoa
ripoti ya huduma yake inavyokwenda na kuwajibika (MATENDO 14:27; 21:17-19; 1WAKORINTHO 14:29).
7.
Miujiza ya Mungu, hutusogeza katika kumtumikia Yesu Kristo na
kushika maagizo yake, na kutufanya kuwa watakatifu kama yeye alivyo
mtakatifu. Miujiza yoyote inayoambatana na maagizo yoyote yaliyo kinyume
na Neno la Mungu, kama kutumia sanamu za watakatifu, kufukiza uvumba,
kutumia rozari au maji ya Baraka, kuzuru makaburi, kuwaomba wafu
tuwaombee n.k; haitokani na Mungu (KUMBUKUMBU 13:1-4).Mafundisho
ya mtu anayetumiwa kufanya miujiza ya Mungu, hutufundisha kuwa
watakatifu, na kuwa mbali na mapenzi ya Mataifa. Wote waliotumiwa sana
na Mungu kufanya miujiza kama Paulo, Petro, Yakobo na Yohana,
walifundisha hivyo (WARUMI 12:1-2; 1YOHANA 2:15-17; 1 PETRO 1:14-16; 2:12; 4:2-3; YAKOBO 4:4; 1 WAKORINTHO 4:3-4).
8. Miujiza ya Mungu hutolewa bure, hainunuliwi (MATHAYO 10:8; 2 WAFALME 5:14-16; DANIELI 5:16-17; 1 WAFALME 13:6-8; MATENDO 8:18-20).
Namna yoyote ya kuomba hela ili kununua muujiza ni kinyume na mpango wa
Mungu .Hata kama tutaona wakiuza vitambaa,leso na sabuni zilizoombewa
ili zitusaidie, hatuna budi kujua mapanzi ya Mungu kwa watumishi wake ni
kutoa huduma ya maombezi bure. Huduma yoyote inayochangisha mchango au
kiingilio kwa ajili ya semina ya Neno la Mungu hiyo siyo huduma ya
kimungu, ni huduma ya Shetani. Mungu anataka injili iwafikie watu
wote.Mfano 1 wa huduma ya shetani ni huduma ya babu wa Loliondo. Bila
kutoa sh: 500 usingeweza kupata msaada.Pia miujiza ya Mungu inatokana
na Neno la Mungu kama tulivyoona hapo juu. Miujiza ya Mungu inakuwa na
lengo la kuwaleta watu kwa Yesu.Watu wanaokuja kutafuta msaada kwa Yesu
sharti waongozwe kutubu dhambi zao
kwanza ili kuwapatanisha na Mungu kwa ajili ya kufungua mlangio wa Miujiza yao.
9. Miujiza ya Mungu humtukuza mwana wa , Yesu kristo (YOHANA 11:4), wale wanaotumiwa na Mungu kufanya miujiza ya Mungu hubaki wanadamu na wao kukiri hivyo, na kumpa Mungu utukufu(MATENDO 14:8-18). Tunapomuona mtu akichukua utukufu kana kwa mba yeye ndiye anayetenda miujiza ndipo tunatambua kuwa huyo si mtumishi wa Mungu.
10. Maisha ya mtu anyetumiwa na Mungu kufanya miujiza
yanapaswa kuwa sawasawa na Neno la Mungu. Watu wanaotumiwa na Shetani
kufanya miujiza, huambatana na dhambi NNE zinazoonekana upesi-uzinzi au
uasherati (1 WAKORINTHO 6:15-17), maneno ya kihuni(YAKOBO 3:10-12), maisha yaliyo sawa na mataifa katika kuvaa na kutenda (WARUMI 12:2; 1 PETRO 2:12; YAKOBO 4:4), maisha yasiyo na uaminifu katika masuala ya fedha na kusema uongo (NEHEMIA 7:2)
3. HUKUMU YA WATUMISHI WA SHETANI
Watumishi wanaotumiwa kufanya miujiza ya mashetani, mahali pao ni katika ziwa la moto (UFUNUO 19:20; KUMBUKUMBU 13:1-5; MATHAYO 7:22-23. Baada ya kuwa tumefahamu; ni wajibu wetu kujihadhari nao na kuwa mbali na mafundisho yao (MATHAYO 7:15-17; WARUMI 16:17).Mungu
akuongoze kufanya maamuzi mazuri katika kuchagua mahali pa kuabudia
(dhehebu au kanisa), maana kufanya makosav katika kuchagua mahali pa
kulishwa NENO LA MUNGU kunaweza kukugharimu milele. Tafuta mahali ambapo utaelezwa kweli yote bila kufarijiwa kunyume na maandiko.
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika
Facebook, Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate
nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa.
Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini
ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi.
Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.
UBARIKIWE NA BWANA YESU!!!







0 comments:
Post a Comment
say something